AZAM BD League Started

Everyone is invited to come and see their stars.

Angola lost to China in 2014 FIBA World Championship for Women

Shao Ting indeed is the perfect representation of the transition in Chinese women's basketball.

FRIDAY Basketball Night

Everyone is invited to Friday Night Fever.

Tuesday, February 17, 2015

Matokeo ya Ligi ya AZAM BD League - Round ya Pili (Week Six)



Tuesday, January 13, 2015

Matokeo ya Michezo yote iliyochezwa juma la kwanza

Ifuatayo ni jedwali linalo onyesha michezo yote iliyo chezwa katika juma la kwanza la mzunguko wa pili wa ligi ya mpira wa kikapu ijulikanayo kama AZAM BD RBAL LEAGUE 2014/15.

Tuesday, December 23, 2014

YAH: MZUNGUKO WA PILI LIGI YA MKOA (AZAM BD LEAGUE) 2015



Chama cha Mpira wa kikapu Mkoa wa Dar Es Salaam kinapenda kuwajulisha wadau wake wote kuwa mzunguko wa pili wa ligi tajwa unatarajiwa kuanza tarehe 9 January 2015 na kumalizika 14 March 2015 baada ya mapumziko yaliyopisha mashindano ya vyuo (SHIMIVUTA) yaliyo malizika hivi karibuni mkoani Tanga na Sherehe za Xmas na Mwaka Mpya.

Hivyo basi michezo ya ligi itachezwa siku za Ijumaa Jioni,Jumamosi na Jumapili chini ya udhamini wa Bakhresa Food Products Ltd kupitia kinywaji chake cha Azam Cola.

Ratiba ya Mzunguko wa pili inapatikana hapa

Monday, December 1, 2014

Temeke Mabingwa - Taifa Cup 2014 Dodoma

Timu pekee ya Temeke kutokea Mkoa wa Dar Es Salaam imefanikiwa kutwaa taji la Taifa Cup 2014 kwenye michuano iliyofanyika Mkoani Dodoma baada ya kuifunga Timu ngumu ya Mkoa wa Mbeya kwa jumla ya vikapu 85 - 43.





AZAM BD LEAGUE - KUKAMILISHA MECHI ZA VIPORO

Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar Es Salaam kinapenda kutoa taarifa kwa vilabu vya JOGOO,DB Young Stars,Kurasini Heats,DB Lioness,Mgulani na Jeshi Stars kuwa michezo yao ya viporo itafanyika tarehe 5 na 6 Desemba 2014 hii inatokana na matumizi ya uwanja kuwa na shughuli za michezo ya Ngumi za Kimataifa.

Tafadahali barua husika za taarifa hii zitawafikia vilabuni kwenu.


Thursday, November 6, 2014

Matokeo ya Ligi AZAM-BD kwa juma la sita

Ligi ya Mpira wa Kikapu inayo ratibiwa na Chama cha Mpira huo jijini Dar Es Salaam imeendelea tena wiki hii kwa michezo kati ya DB Lioness na JKT Stars ambapo timu ya JKT Stars iliibuka na ushindi wa vikapu 71-35 na Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Oilers vs CHUI ambapo mchezo haukumalizika kutokana na kukatika kwa umeme huku timu ya CHUI ikiwa mbele kwa vikapu 35-17 dhidi ya Oilers ndani ya kipindi cha tatu cha mchezo,hata hivyo kamisaa aliuhairisha mchezo mpaka taarifa ya marudiano itakapo tolewa.

Siku ya Jumamosi ligi iliendelea kwa michezo ya Vijana Queens na Tanzania Prisons (wanawake) na Vijana Queens kuibuka na ushindi mwembamba katika mchuano mkali wa vikapu 75-74 ,Timu ya  ya PAZI ilifanikiwa kuifunga Timu ya DB Young Stars kwa jumla ya vikapu 86-71,Timu ya Jogoo ilifanikiwa kuifunga timu ya TZ Prisons (Wanaume) kwa vikapu 75-59.
Siku ya Jumapili ligi ya mpira wa kikapu iliendelea kwa michezo minne ambayo ilikuwa ni kati ya TZ Prisons Queens dhidi ya Jeshi Stars ambapo Prisons Queens walishinda kwa vikapu 62-55, Mchuano mkali kati ya Timu ya Savio na JOGOO ulimalizika kwa timu ya SAVIO kuibuka kidedea kwa ushindi mwembamba wa point moja (77-76) kwenye mchezo ulio kuwa na hamasa za aina mbalimbali,Timu ya Oilers nayo ilifanikiwa kuifunga timu inayo chipukia ya DB Young Stars kwa vikapu 83-77,Mchezo wa mwisho ulikuwa ni kati ya Chang'ombe United vs Vijana City Bulls ambapo vijana iliibuka mshindi kwa vikapu 69 - 53.

Friday, October 31, 2014

MABADILIKO YA SHERIA ZA MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU-2014

BAREDA inajulisha wadau wote kutambua si sheria zote za mchezo wa mpira wa kikapu zilizobadilishwa, watambue kuwa ni marekebisho Machache yasiozidi Matano yenye uhusiano wa moja kwa moja na yanayoweza kuleta athari kwa Teams zinapokuwa mchezoni.

Marekebisho mengine ni ya kiutawala hasa kwa waamuzi na hayana athari kwa Teams zinapocheza mfano Signalling-namna ya kuripoti kwa kutumia ishara, na matumizi ya Video Replay system kwenye maamuzi bahati mbaya kwenye Ligi zetu Mfumo huu bado Haujaanza kutumika. Furaha zaidi ni kwa wachezaji wanaopenda kuvaa jezi namba zozote ila iwe kati ya 0, 00  hadi  99 ruksa.

BAREDA imejaribu kueleza Pia sababu kwa nini yalifanyika marekebisho ya sheria/articles hizo.

Pakua taarifa hiyo HAPA


Zimeambatanishwa kwa lugha ya kiingereza kulinda Content/Maana isiharibike, Endapo wadau watahitaji zitazifafanuliwa kwa Lugha yetu ya Taifa Kiswahili.

Gosbert
Mwenyekiti BAREDA