Monday, October 13, 2014

Matokeo ya Ligi AZAM-BD kwa juma la tatu

Timu ya Chang'ombe wakipokea maelekezo

Ligi ya Mpira wa Kikapu inayo ratibiwa na Chama cha Mpira huo jijini Dar Es Salaam imeendelea tena wiki hii kwa michezo kati ya Jeshi Stars na JKT Stars ambapo timu ya Jeshi Stars iliibuka na ushindi wa vikapu 66-63 na Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Vijana Queens na DB Lioness ambapo DB Lioness waliibuka washindi kwa jumla ya vikapu 68 -33 vya Vijana Queens.
Wachezaji wakipeana maelekezo

Siku ya Jumamosi ligi iliendelea kwa michezo miwili ambayo ni Chang'ombe na Jogoo ambapo Jogoo waliibuka washindi kwa jumla ya vikapu 80-47,DB Oysterbay Young Stars walipimana ubavu na Timu ya Jeshi la Magereza na Magereza kuibuka washindi kwa jumla ya vikapu 71-61 vya DB Young Stars.

Kocha aifanya interview
Siku ya Jumapili ligi ya mpira wa kikapu iliendelea kwa michezo mitatu ambayo ilikuwa ni kati ya Chang'ombe United na Kurasini Heats timu zote zikitokea wilaya ya Temeke kwa Kurasini Heats kuibuka na ushindi wa vikapu 57-53 vya Chang'ombe,Mchezo mwingine ulizikutanisha timu machachari nazo zikitokea wilaya moja ya Kinondoni (Kama zilivyokutana kwenye fainali ya mchezo huo ngazi ya wilaya) kati ya PAZI na CHUI ambapo hadi mwisho wa Mchezo PAZI iliibuka kifua mbele kwa ushindi wa vikapu 72-60 vya Chui,Mchezo mwingine ulizikutanisha OILERS na timu ya VIJANA na VIJANA kufanikiwa kuifunga OILERS kwa jumla ya vikapu 57-45.