Chama cha Mpira wa kikapu Mkoa wa Dar Es Salaam kinapenda kuwajulisha wadau wake wote kuwa mzunguko wa pili wa ligi tajwa unatarajiwa kuanza tarehe 9 January 2015 na kumalizika 14 March 2015 baada ya mapumziko yaliyopisha mashindano ya vyuo (SHIMIVUTA) yaliyo malizika hivi karibuni mkoani Tanga na Sherehe za Xmas na Mwaka Mpya.
Hivyo basi michezo ya ligi itachezwa siku za Ijumaa Jioni,Jumamosi na Jumapili chini ya udhamini wa Bakhresa Food Products Ltd kupitia kinywaji chake cha Azam Cola.
Ratiba ya Mzunguko wa pili inapatikana hapa