AZAM BD League Started

Everyone is invited to come and see their stars.

Angola lost to China in 2014 FIBA World Championship for Women

Shao Ting indeed is the perfect representation of the transition in Chinese women's basketball.

FRIDAY Basketball Night

Everyone is invited to Friday Night Fever.

Thursday, November 6, 2014

Matokeo ya Ligi AZAM-BD kwa juma la sita

Ligi ya Mpira wa Kikapu inayo ratibiwa na Chama cha Mpira huo jijini Dar Es Salaam imeendelea tena wiki hii kwa michezo kati ya DB Lioness na JKT Stars ambapo timu ya JKT Stars iliibuka na ushindi wa vikapu 71-35 na Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Oilers vs CHUI ambapo mchezo haukumalizika kutokana na kukatika kwa umeme huku timu ya CHUI ikiwa mbele kwa vikapu 35-17 dhidi ya Oilers ndani ya kipindi cha tatu cha mchezo,hata hivyo kamisaa aliuhairisha mchezo mpaka taarifa ya marudiano itakapo tolewa.

Siku ya Jumamosi ligi iliendelea kwa michezo ya Vijana Queens na Tanzania Prisons (wanawake) na Vijana Queens kuibuka na ushindi mwembamba katika mchuano mkali wa vikapu 75-74 ,Timu ya  ya PAZI ilifanikiwa kuifunga Timu ya DB Young Stars kwa jumla ya vikapu 86-71,Timu ya Jogoo ilifanikiwa kuifunga timu ya TZ Prisons (Wanaume) kwa vikapu 75-59.
Siku ya Jumapili ligi ya mpira wa kikapu iliendelea kwa michezo minne ambayo ilikuwa ni kati ya TZ Prisons Queens dhidi ya Jeshi Stars ambapo Prisons Queens walishinda kwa vikapu 62-55, Mchuano mkali kati ya Timu ya Savio na JOGOO ulimalizika kwa timu ya SAVIO kuibuka kidedea kwa ushindi mwembamba wa point moja (77-76) kwenye mchezo ulio kuwa na hamasa za aina mbalimbali,Timu ya Oilers nayo ilifanikiwa kuifunga timu inayo chipukia ya DB Young Stars kwa vikapu 83-77,Mchezo wa mwisho ulikuwa ni kati ya Chang'ombe United vs Vijana City Bulls ambapo vijana iliibuka mshindi kwa vikapu 69 - 53.

Friday, October 31, 2014

MABADILIKO YA SHERIA ZA MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU-2014

BAREDA inajulisha wadau wote kutambua si sheria zote za mchezo wa mpira wa kikapu zilizobadilishwa, watambue kuwa ni marekebisho Machache yasiozidi Matano yenye uhusiano wa moja kwa moja na yanayoweza kuleta athari kwa Teams zinapokuwa mchezoni.

Marekebisho mengine ni ya kiutawala hasa kwa waamuzi na hayana athari kwa Teams zinapocheza mfano Signalling-namna ya kuripoti kwa kutumia ishara, na matumizi ya Video Replay system kwenye maamuzi bahati mbaya kwenye Ligi zetu Mfumo huu bado Haujaanza kutumika. Furaha zaidi ni kwa wachezaji wanaopenda kuvaa jezi namba zozote ila iwe kati ya 0, 00  hadi  99 ruksa.

BAREDA imejaribu kueleza Pia sababu kwa nini yalifanyika marekebisho ya sheria/articles hizo.

Pakua taarifa hiyo HAPA


Zimeambatanishwa kwa lugha ya kiingereza kulinda Content/Maana isiharibike, Endapo wadau watahitaji zitazifafanuliwa kwa Lugha yetu ya Taifa Kiswahili.

Gosbert
Mwenyekiti BAREDA

Thursday, October 30, 2014

MABADILIKO YA RATIBA SIKU YA IJUMAA TAREHE 31/10/2014

Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar Es Salaam kinapenda kutangaza mabadiliko madogo ya Ratiba siku ya Ijumaa tarehe 31/10/2014 ambayo yameangalia nafasi za kila timu kuweza kupata muda wa kuonekana live kama sehemu ya kuutangaza mchezo kwa kuonyesha michezo tofauti yenye viwango na msisimko tofauti ili kuongeza hamasa na msisimko kwa watazamaji watakao angalia moja kwa moja kupitia Television ya AZAM TV.

Hivyo kutokana na mabadiliko haya michezo ifuatayo itachezwa siku ya ijumaa na jumamosi.

Ijumaa - 31/10/2014
1800hrs - JKT Stars vs DB Lioness
2000hrs - TZ Prisons vs JOGOO

Jumamosi - 1/11/2014
1600hrs - Oilers vs CHUI

Vilabu vitakavyo guswa na mabadiliko haya vinaombwa kuzingatia mabadiliko husika.

Imetolewa na Kurugenzi Ufundi
Jimmy D. Nkongo

TAMKO LA BAREDA/OFFICIAL STATEMENT

BAREDA inaandaa ripoti ya Mashindano (AZAM RBA LEAGUE 2014/15 REVIEW REPORT-FIRST ROUND) ambayo itatoa taarifa za kina na zisizo na upendeleo kwa upande wowote kwa mambo mbali mbali yaliyojitokeza, Changamoto, na Way forward, Hasa kwa Upande wa Officiating/Referee na kuikabidhi kwa Mkurugenzi Mtendaji BD.

BAREDA inawapongeza Waamuzi kwa kazi nzuri pia kuwa makini , watulivu na inapobidi kuwa kimya kwani Maadili ya uamuzi (Official Ethics ) yanatuhitaji kuwa hivyo,  Pamoja na mazingira magumu itaendelea na tabia hii na kutoa ushirikiano mzuri na wa kiwango cha juu kwa wadau wote wa mchezo wa kikapu.

BAREDA inawashukuru baadhi ya makocha na wadau wengi  wanaotoa ushirikiano mzuri kwa waamuzi na mawazo mazuri wanayoleta kuhusu Uboreshaji, pia na wao Kupokea maoni yetu kuhusu tafsiri mbali mbali za sheria  za mchezo, tunajisikia Faraja sana kuona Mnafanyia kazi Ushauri wetu, Ushirikiano huu mzuri wa kujadili mambo uendelee pia katika mzunguko wa pili.

Tunatanguliza Shukurani zetu,
WE ARE BASKETBALL

Gosbert.
M/KITI- BAREDA

Tuesday, October 28, 2014

Semina ya siku moja juu ya sheria mpya za kikapu 2014

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kupitia kamisheni zake za Ufundi na Uendeshaji Mashindano na Waamuzi linapenda kukutaarifu kuwa  limeanda semina ya siku1 kama ilivyoelezwa hapo juu.

Semina hii ni kwa ajili ya waamuzi wote wa DSM,Waalimu wa Timu,wachezaji na Viongozi wote wa Vilabu DSM itafanyika TAR:31/10/2014 SAA 6 MCHANA UWAJA WA TAIFA WA NDANI.Lengo kama chama kilicho na Dhamana ya kusimamia mchezo wa Mpira wa Kikapu nchini kinatakiwa kuzitafasiri na kuruhusu kuanza kuzitumi rasmi sheria hizi mpya katika raundi ya pili ya ligi ya AZAM-BD  na Taifa cup 2014/November - Dodoma

Nimatarajio ya chama utashirikiana nasi katka kuendeleza Mpira wa Kikapu Tanzania.Pia chama baada ya kuona malalamiko mengi kwa uchezeshaji wa waamuzi kitakaa kupitia wajumbe wake wa kamisheni hizi 2 kuona jinsi watakavyo andaa muharubaini wa tatizo hili na kulipatia ufumbuzi wa haraka.

Taarifa hizi zimetolewa kwenu na:-

Manasseh Zablon Mghamba                                         
Kaimu Kamishna wa waamuzi (TBF)
Kamishina wa Ufundi na Uendeshaji Mashindano (TBF)
0787/0712 1937 66/0754 26 3615.

Nakala:BMT,PATRON TBF,VILABU VYOTE BD

Wednesday, October 15, 2014

Taarifa za Mkutano na Wadau (Waamuzi,Viongozi wa Vilabu na Ma-Kaptain) - Alhamisi 16 Oktoba 2014

Basketball Dar Es Salaam (BD) inapenda kuwataarifu wadau ambao ni Waamuzi wote wa mchezo wa Mpira wa Kikapu,Viongozi wa Vilabu na Ma-Captains wote kuwa kutakuwa na mkutano siku ya alhamisi tarehe 16 Oktoba 2014 Don Bosco Upanga kujadili maendeleo ya ligi pamoja  na changamoto zake.

Mkutano huu utaanza rasmi saa 1700hrs (Kumi na moja jioni) hivyo sote tunashauriwa kuhudhuria bila kukosa ili mawazo na mapendekezo yetu sote kwa pamoja yajadiliwe na hatimaye kufanyiwa kazi.

Upatapo taarifa hizi mjulishe na mwamuzi,kiongozi au Captain mwenzako.

Taarifa hii imetolewa na :-
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji

Monday, October 13, 2014

Miaka 15 ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Letu

Baba wa Taifa Mwl.Julius K. Nyerere inasemekana alipenda sana Mchezo wa mpira wa Kikapu (Basketball) yeye pamoja na Raisi wetu wa sasa Mh. Dkt. Jakaya M. Kikwete wakifurahia jambo kwenye uzinduzi wa ligi ya SUPER CUP.

Hivyo basi mwaka huu (2014) kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 15 ya kumbumbu ya kifo chake.

Tanzania Basketball Federation (TBF) iliandaa shindano la kuenzi mchango wake kwenye maendeleo ya Taifa letu.Mshindi wa shindano hilo atazawadiwa zawadi ya kombe lililotolewa na mjumbe wa NEC kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Phares Magessa kwa mujibu wa maelezo yaliyo tolewa na Katibu Mkuu wa TBF,Bw. Saleh Zonga.

Shindano hilo limeshafanyika mjini Musoma kwa timu ya JKT kutwaa taji la ubingwa baada ya kuzishinda timu zote zilizo shiriki shindano hilo ambazo ni Profile - Mwanza,Mwembeni 1 & 2 ,Makoko - Musoma.