Monday, October 6, 2014

Matokeo ya Ligi AZAM-BD kwa juma la pili

 Ligi ya Mpira wa Kikapu inayo ratibiwa na Chama cha Mpira huo jijini Dar Es Salaam imeendelea tena wiki hii kwa michezo kati ya Vijana na Mgulani ambapo timu ya Mgulani JKT iliibuka na vikapu 57-46 na Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Jogoo na DB Young Stars ambapo DB Young Stars waliibuka washindi kwa jumla ya vikapu 75-73 vya Jogoo.

Siku ya Jumamosi ligi iliendelea kwa michezo minne ambayo ni Chang'ombe na Pazi ambapo PAZI ambao ni mabingwa wa wilaya ya Kindononi waliibuka washindi kwa jumla ya vikapu 66-57,Oilers walipimana ubavu na Timu ya Savio (ambao ni mabingwa wa wilaya ya Ilala) na SAVIO kuibuka washindi kwa jumla ya vikapu 64-63 vya Oilers,Mchezo mwingine ulikuwa ni mchezo wa wanawake kati ya Timu ya Jeshi Stars dhidi ya Vijana Queens ambapo Jeshi Stars walishinda kwa vikapu 67-35 na mchezo wa mwisho siku ya Jumamosi ulikuwa kati ya Timu ya Magereza iliyo chuana vikali na Timu ya JKT (Mabingwa wa Taifa) ambapo JKT waliweza kudhihirisha ubabe wao kwa ushindi wa vikapu 67-43.



Siku ya Jumapili ligi ya mpira wa kikapu iliendelea kwa michezo minne ambayo ilikuwa ni kati ya Vijana na Jogoo timu zote zikitokea kwenye Klabu Moja kwa Vijana kuibuka na ushindi wa vikapu  68-65,Mchezo mwingine ulizikutanisha timu machachari na ndio zilizo panda daraja kwa mara ya kwanza kushiriki kwenye ligi hii ya Mkoa wa Dar Es Salaam ijulikanayo kama AZAM -BD League,ulikuwa ni kati ya Mgulani JKT na Don Bosco Young Stars ambapo hadi mwisho wa Mchezo DB Young Stars iliibuka kifua mbele kwa ushindi wa vikapu 58-56,Mchezo mwingine ulizikutanisha PAZI na timu ya Magereza na PAZI kufanikiwa kuifunga Magereza jumla ya vikapu 73-40,Mchezo wa Mwisho ulikuwa kati ya Chang'ombe na JKT ambapo timu ya JKT iliendeleza ubabe wake kwa kuifunga bila huruma timu ya Chang'ombe United kwa jumla ya vikapu 92-38